Rais wa Marekani, Donald Trump anajipanga kuiwekea vikwazo nchi ya China mara baada ya kugundua kuwa nchi hiyo imekuwa ikiiba utaalam na ubunifu wa biashara za Marekani.
Ikulu ya Marekani imesema kuwa hatua hiyo imefikiwa mara baada ya kufanyika mazungumzo ya muda mrefu bila kufikia muafaka kuhusu jambo hilo.
Aidha, Mpango huo umezua hofu kubwa kuhusu vita vya kibiashara kati ya nchi hizo kwani vikwazo hivyo vitashirikisha ushuru na masharti mengine.
Vilevile huenda Marekani ikawasilisha malalamiko yake kwa Shirika la Biashara Duniani WTO, kulingana na maafisa wa biashara.
Hata hivyo, Bunge la Congress pia linapanga kupitisha sheria ambayo itaipatia serikali uwezo wa kubadilisha mikataba ya biashara za kigeni kutokana na vitisho vya China kununua viwanda vya Marekani.
-
Uingereza yaruhusu mtoto kupewa bangi
-
Msichana aliyewapiga makofi wanajeshi wenye bunduki afungwa jela
-
Wabunge wa upinzani wafyatua gesi ya machozi bungeni