Hatimaye Serikali ya Uingereza imewaruhusu Wazazi wa mtoto mwenye umri wa miaka 6, Alfie Dingley anayesumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kumpa bangi kama tiba ya ugonjwa huo.

Wakizungumza mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu, Theresa May, Drew Dingley na Hannah Deacon wamesema kuwa wameambiwa kijana wao Alfie anaweza kuruhusiwa kutumia mafuta yatokanayo na mmea wa Bangi kwa makubaliano maalumu ingawa matumizi ya Bangi ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Alfie Dingley huanguka kifafa mara mia moja na zaidi kila mwezi lakini hali hiyo inaweza kupungua ikiwa atapewa matone matatu ya bangi kwenye ulimi kila siku.

Hata hivyo, Mama mzazi wa mtoto huyo ameelezea tabu anazozipata, jaziba na hasira ambazo mtoto huyo anamfanyia kutokana na matatizo ya maradhi yake ya kifafa.

Mario Balotelli huenda akarejeshwa kikosini
Mmoja atiwa mbaroni shambulio la afisa wa Syria