Jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni linamshikilia mtumishi mmoja wa ubalozi wa Syria kufuatia kuvamiwa kwa Afisa wa ubalozi huyo hapa nchini, Hassan Alfaouri na kuporwa fedha kiasi cha Euro 9300 sawa na Milioni 25 za KItanzania.

Taarifa hiyo ni kufuatia taarifa ya kushambuliwa kwa Afisa ubalozi wa Syria nchini Tanzania na watu watatu wasiojulikana na kupigwa na kuporwa  simu na gari aliyokuwa akiitumia kwa shughuli za ubalozi.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abasi amefunguka na kukiri kutokea kwa shambulio hilo la kijambazi na kudai kuwa serikali inafuatilia na itatoa taarifa kamili kuhusu jambo hilo.

“Umma unaarifiwa kuwa vyombo vya dola vinafuatilia taarifa za Afisa Ubalozi wa Syria nchini kushambuliwa, kuporwa. Taarifa kamili itatolewa” amesema Abasi

Aidha katika taarifa za awali zinadai kuwa afisa huyo amelazwa katika hospitali ya Agha Khan akipatiwa matibabu kufuatia shambulio hilo.

Uingereza yaruhusu mtoto kupewa bangi
Necta yafanya mabadiliko mtihani darasa la saba