Rais wa Marekani Donald Trump amekanusha tuhuma kwamba anampango kumfukuza kazi mwendesha mashtaka maalum wa nchi hiyo, Robert Mueller ambaye amekuwa akiongoza uchunguzi kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

Mvutano mkali umekuwa ukiongezeka kadri siku zinavyokwenda kati ya Ikulu ya Marekani na mwendesha mashtaka huyo, Mueller na maafisa uchaguzi wa Trump wa mwaka 2016 nchini Marekani.

Akijibu maswali kuhusu mgogoro huo wa kisheria, Trump amesema kuwa hali si nzuri sana kwani mawakili wake wamejawa na ghadhabu.

“Siwezi nikafikiria kwamba kuna chochote kinachoendelea kwa sababu, kama tulivyosema, hatukushirikiana na Urusi katika uchaguzi mkuu uliopita,”amesema Trump

Hata hivyo, Utawala wa Donald Trump umekanusha vikali tuhuma kuwa ulishirikiana na Urusi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2016, rais huyo amesema tuhuma hizo ni kutaka kumchafua kisiasa.

 

 

Zitto aiwashia moto Takukuru
Video: Lissu amsubiri ndugai kwa hamu, Mangula arudishwa