Rais wa Marekani Donald Trump ametengua uteuzi wa Waziri wa Ulinzi wa Nchi hiyo Mark Esper, hii ikiwa baada ya wawili hao kutofautiana hadharani katika wiki za hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Trump ametangaza kuwa nafasi ya afisa huyo wa ngazi ya juu wa Marekani itakaimiwa na Christopher Miller, mkuu wa sasa wa Kituo Cha kukabiliana na ugaidi.
Uamuzi wa Trump unakuja siku mbili baada ya mpinzani wake Joe Biden kushinda uchaguzi na kutangazwa kuwa Rais Mteule wa Marekani.
Trump mpaka sasa hajakubali kushindwa katika uchaguzi wa Marekani na rais mteule Joe Biden, na ameapa kupinga matokeo hayo mahakamani zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya Biden kuchukua ofisi Januari 20.
Kulingana na Sheria za Marekani, Trump bado ana uwezo wa kufanya maamuzi.