Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka watendaji ndani ya serikali kuchapa kazi na kuachana na wasiwasi wa kuhisi atawaondoa.

Magufuli ameyasema hayo leo Novemba 9, 2020. wakati akitoa hotuba yake baada ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

“Wakuu wa mikoa na wilaya msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko yoyote labda kwa atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo, kama nilikuteua uwezo si bado ni ule ule najua wananisikia wachape kazi wasipochapa kazi shauri yao”, amesema Magufuli.

“RC unakuwa na wasiwasi gani labda kama ‘performance’ yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nashangaa napata vimeseji kwamba Mheshimiwa Rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa”, – ameongeza Rais Magufuli.

Ndayiragije: Nimewafuatilia Tunisia
Lema akamatwa na polisi