Ikulu ya Rais wa Marekani ya White House imeyazuia Mashirika Makuu ya habari nchini humo kuhudhuria kikao cha wanahabari kilichoendeshwa na msemaji wa Ikulu.
Wanahabari wa Mashirikia ya CNN, The New York Times, Politico, Los Angeles Times na BuzzFeed hawakuruhusiwa kuhudhuria kikao cha wanahabari katika ofisi ya msemaji wa Ikulu ya Rais wa Marekani Sean Spicer.
Aidha, utawala wa Rais Donald Trump umekuwa ukiyashutumu mashirika hayo kuwa yanaeneza habari za uongo na za kupotosha, Spicer hakutoa maelezo kwanini waandishi wa habari wa mashirika hayo waliachwa nje ya kikao kisicho rasmi cha wanahabari, hatua ambayo imeibua shutuma kali.
Hata hivyo, Shirika la habari la Reuters pamoja na mashirika mengine 10 yakiwemo Bloomberg na CBS yameruhusiwa kuhudhuria mkutano huo wa wanahabari, Wakati wanahabari kutoka CNN na mashirika mengine yaliyozuili yalipojaribu kuingia IKulu, yalizuiwa kwa kuambiwa majina yao hayako katika orodha ya wanahabari walioalikwa.