Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kusitisha misaada kwa taifa la Palestina iwapo litakataa kushiriki katika mazungumzo ya amani.
Ameyasema hayo wakati akizungumzia masuala ya kiuchumi ambapo ametanabaisha kuwa Palestina imekuwa ikiivunjia heshima Marekani.
Amesema kuwa Marekani inawapatia Palestina mamilioni ya dola kama msaada wa mambo mbalimbali kila mwaka ili kuiwezesha nchi hiyo kufanya shughuli zake.
”Hizo pesa ambazo huwa tunawapatia Palestina ziko mezani, lakini hazitawafikia hadi pale watakapokubali kukaa meza moja ya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu,”amesema Trump
Hata hivyo, Trump amethibitisha kuwa Israel inataka kuanza mazungumzo ya amani na Palestina ili kuweza kupata suluhu ya mgogoro huo ambao umedumu kwa muda mrefu.