Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, amesema kuwa atampa haki zake zote za msingi aliyekuwa rais wa nchi Robert Mugabe na mkewe.

Amesema kuwa Mugabe ataendelea kupokea mshahara wake na mafao mengine kama kawaida ikiwemo kusafiri katika daraja la kwanza kwenye ndege (first class), pamoja na kusafiri kwa gharama ya serikalI.

Aidha, amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria kwani mtu yeyote anaweza kushtakiwa na ameongeza kuwa kwa sasa nchi hiyo inafanya mpango wa kujiunga tena na mataifa ya Jumuiya ya Madola.

‘Hatujampa kinga mtu yoyote isipokua ambacho nimeahidi kwa rais aliyetangulia na baba wa taifa letu, rais Robert Mugabe ni kwamba tunampatia mafao na mshahara wake kama alivyokua akipata awali, usafiri, ofisi, ulinzi, na serikali yangu itamuwezesha kwenda Singapore kwenye matibabu, na vyote hivi mke wake pia ataviapata,”amesema Rais Mnangagwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa serikali yake mpya inafanya jitihada kubwa za kupambana na rushwa ambayo amesema kuwa hawezi kuivumilia hata kidogo.

 

 

 

Waamuzi wa Tanzania walamba dili CAF
Video: Tundu Lissu nimetolewa risasi nyingine mwilini, Wabunge 11 wasota kizimbani