Rais wa Marekani Donald Trump ametoa msaada wa mashine za kusaidia wagonjwa kupumua (ventilators) katika nchi za bara la Afrika na kusema kwa sasa wana uwezo wa kusaidia nchi nyingine hivyo amefungua njia kwa nchi zenye uhitaji.
Trump amesisitiza kuwa ni muhimu kwa nchi mbambali kuongeza juhudi katika kuwapima watu wake virus vya corona huku akitolea mfano wa Marekani ambapo mpaka sasa imewapima Watu wengi hadi kufikia hivi sasa.
“Ni kujidanganya kwa kuamua kusema una idadi ndogo ya visa vya corona wakati kiwango cha upimaji kipo chini, Marekani sasa tumewapima zaidi ya Watu Million 5, hii ni zaidi ya Nchi yoyote Duniani na hata Mataifa makubwa yakiungana idadi ya Watu waliowapima haitufikii”amesema Rais Trump.
Ameongeza kuwa ”Marekani ina Ventilators za kutosha, na ameongea na Waziri Mkuu Ethiopia Barani Afrika, Nchi yao inataka ventilators, tutawapa”