Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Aprili 27, 2020 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula kwa kusumbuliwa na maradhi ya Moyo.

Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda, kimetokea alfajiri ya kuamkia leo baada ya kuugua kwa siku mbili.

Mmanda aliteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mtwara na Rais Magufuli Desemba 19, 2016 akichukua nafasi ya Dkt. Khatib Kazungu ambaye alihamishiwa Wizara ya Fedha.

Trump atoa msaada mashine za kupumua wenye Corona Afrika
Ikulu ya Korea Kusini yatoa tamko kuhusu afya ya Kim Jong-un, ‘yuko hai’