Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wa mataifa ya Afrika.
Viongozi hao wamekutana mjini Davos, Uswizi katika kongamano la uchumi na biashara duniani, ambapo mkutano huo wa Kagame na Trump umetokea mara baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuyaita mataifa ya Afrika kuwa ni mataifa ya mabwege.
“Napenda kukupongeza, Rais Kagame kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa AU, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa, najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza hivi karibuni. taafadhali fikisha salamu zangu kwa mataifa yote ya Afrika,”amesema Trump
Hata hivyo, Rais Kagame amesema kuwa wameshauriana masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya watalii wa Marekani nchini Rwanda.