Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa hana matumaini ya kuendelea na mkaba wa biashara huria (NAFTA) unaoundwa na nchi za Marekani, Mexico na Canada.
Katika mazungumzo yake na waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau ya kuujadili mkaba huo uliodumu kwa muda wa miaka 20 hawakuweza kufikia makubaliano hivyo kila mmoja kuondoka bila majibu.
Aidha, Trump amesema kuwa Marekani, Mexico na Canada huenda zisifikie makubaliano katika kuujadili upya mkataba huo wa biashara huria katika mataifa ya Amerika ya kaskazini, hivyo waanze kuangalia utaratibu mwingine.
Kwa upande wake waziri mkuu wa Canada amesema kuwa bado anamatumaini makubwa ya kuunusuru mkataba huo kuvunjika, kwani nchi hizo bado zina uhusiano mzuri wa kibiashara.
-
Kenyatta amjibu Raila baada ya kujiondoa mbio za urais
-
Uchanguzi Kenya bado kitendawili
-
Trump kufuta leseni za vyombo vya habari Marekani
“Tuna mahusiano ya karibu, nchi zote mbili zina uhusiano wa kiuchumi, utamaduni na mahusiano baina ya watu wake. Lakini tuna mahusiano mazuri siku zote na kuna njia ya kuyaboresha. Masuala yote haya tunapaswa kuyazungumzia na ndio maana tuko na mahusiano ya kujenga kati ya rais na waziri mkuu, ni muhimu na nimefurahi kukutana na wewe tena hii leo,”amesema Trudeua