Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amepokea mwaliko kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump kumuhitaji aende nchini Marekani mwezi ujao ili waweze kujadiliana kuhusiana na uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Katika  taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini Israel, Netanyahu amesema mwaliko huo ni muhimu kwake kwani anatumai utaweza kumsaidia kupata ushauri ya nini kifanyike ili eneo la Mashariki ya kati liwe na amani.
Mkutano huo baina ya Trump na Netanyahu unakuja siku chache baada ya baadhi ya viongozi wakuu wa nchini  Israel kuidhinisha ujenzi wa nyumba 560 kwa ajili ya walowezi, mashariki mwa Jerusalem.
Ujenzi huo kwa namna moja ama nyingine unadaiwa utachochea uhasama uliopo hivi sasa baina ya Waisraeli na Wapalestina  ambapo Wapalestina wanatumai kuwa Jerusalem Mashariki itakuwa mji mkuu wa taifa lao litakapoundwa siku zijazo.

Zinedine Zidane Aingia Majaribuni
Video: Tanzania yalamba dume Uturuki, Ukawa yashangaa