Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi  leo Juni 11, 2019 jijini Dodoma amezungumza na Mashirika/ Taasisi na makampuni 207 yanayodaiwa kodi ya pango la ardhi ambapo Serikali inadai zaidi ya shilingi bilioni 200 za kodi yake ya ardhi.

Katika Mashirika hayo, TTCL na TANESCO wametajwa kuwa wanaongoza kwa kuwa na deni kubwa ambapo TTCL inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 40 ya kodi ya ardhi na TANESCO ambayo inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 25.

Taasisi nyingine zinazodaiwa ni pamoja na NARCO, NHC, VETA, SUA, UDSM, Kariakoo, puma energy, GAPCO, MSD, CRDB, ATCL, PSPF, Bugando Medical Centre, NMB, TANROADS.

Aidha, Katika hotuba yake, Waziri Lukuvi amesema wadaiwa wote hao watatakiwa kulipa kodi hiyo kabla ya juni 20 na mwisho wa zoezi hilo la kulipa madeni hayo ni Novemba ili kuepuka hatua za kisheria zitakazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kutaifisha mali zao.

 

 

 

Je unatafuta ajira?, Hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako
Mahakama yatoa hati ya kumkamata Wema Sepetu