Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama ameitaka jamii kupanda miti kuzunguka maeneo yenye miradi, ili kuhifadhi mazingira na kuifanya kuwa endelevu.

Mkama ameyasema hayo katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mfumo Mfumo Ikolojia Vijijini – EBARR, katika Wilaya ya Kaskazini ‘A‘ Mkoa wa Kaskazini, Unguja – Zanzibar tarehe 19 Agosti, 2023.

Amesema ameridhishwa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa visima, majengo ya vituo vya wajasiriamali wa ufugaji, ushonaji, utengenezaji wa sabuni na vitalu katika Shehia za Jugakuu na Mbuyutende, huku akiwahimiza viongozi wa shehia hizo kuwasimamia wananchi kupanda miti na kuimwagilia.

“Binafsi nimeridhishwa na namna mnavyosimamia miradi hii na nawapongeza masheha kwa kuisimamia na wananchi kwa kuipokea na kushiriki kikamilifu katika kuitekeleza, niwaombe mhakikishe inaendelea kuwa na ubora ule ule,“ amesisitiza,” amesisitiza Mkama.

Wachimbaji wa Madini waendelea kuchota Madini China
40 ya Kibaka mpapasaji, mpiga mabusu yafikia tamati