Wakufunzi wote wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania waliotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia hivi karibuni isipokuwa Kocha Mkuu, Jorge Vi wamejiuzulu kutokana na tuhuma zinazomkabili Rais wa Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF), Luis Rubiales, za kumbusu mshambuliaji, Jenni Hermoso mdomoni baada ya kutwaa Kombe la Dunia la Wanawake mjini Sydney hivi karibuni.

Makocha wasaidizi Montse Tome, Javier Lerga na Eugenio Gonzalo Martin, pamoja na mtaalam wa fiziki, Blanca Moraleda na kocha wa makipa, Carlos Sanchez, wote wamejiuzulu. Wengine sita wanaohusika na mambo mbalimbali katika benchi hilo pia wamejiuzulu.

Taarifa ya wakufunzi hao, imeeleza: “Wale waliotajwa hapa chini wanalaani vikali tabia iliyooneshwa na rais wa RFEF.” Alitoa hadithi ambayo haiakisi kwa njia yoyote kile kilichohisiwa na Jenni Hermoso, ambaye amesema waziwazi kwamba alihisi kuwa ʻmwathirika wa uchokozi”.

“Kutokana na misimamo na kauli zisizokubalika zinazotolewa na rais, wamefanya uamuzi wa kujiondoa katika majukumu yao” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kocha Mkuu wa timu ya wanaume ya Hispania, Luis de la Fuente naye alisema: “Tabia ya Luis Rubiales hailuheshimu itifaki ya hini kabisa ambayo lazima ifuatwe katika viterndo hivi vya kusherehekea.

“Hazimjengi mtu aliyekuwa anawakilisha soka la His paria. Yeye mwenyewe amekiri hadharani kutofaa kwa tabia yake,” alisema De la Fuente.

Lidha ya Hermoso mwenye umri wa miaka 33 kueleza kuwa busu hilo halikuwa la ridhaa, lakini ufafanuzi huo unapingwa vikali na Rubiales.

Mwishoni mwa juma lililopita, Hermoso anayekipiga Pachuca ya Mexico alitoa taarifa ndefu kwenye mitandao ya kijamü, akisema “Ninahisi haja ya kuripoti tukio hili kwa sababu naamini hakuna ntu, katika kazi yoyote, michezo au mazingira ya kijami anayepaswa kuwa muathirika wa aina ya tabia zisizo za ridhaa.

Young Africans yaivutia kasi Al Merreikh
Mashujaa FC kutafuta makali zaidi Burundi