Aliyekuwa katibu wa chama cha Jubilee nchini Kenya, Raphael Tuju amesema Naibu rais William Ruto alilipwa 2013 kabla ya kumuunga mkono Uhuru Kenyatta.

Tuju amesema hayo katika mahojiano na Radio Inooro, ambapo ameeleza kuwa Ruto ni kiongozi wa vitisho.

“Watu wa mlima wa Kenya wasidhani kuwa Ruto alimuunga mkono Uhuru kwa hiari, kwanza huyu ni mtu wa uhuni, alilipwa, ninaweza kuthibitisha mbele ya Mahakama jinsi ilivyokuwa,” amesema Raphael Tuju.

Tuju aliongeza kuwa kiongozi huyo wa UDA alitaka kulipwa kwanza kabla ya kukubali kuunga mkono Uhuru Kenyatta.

“Alikuja na masharti ambayo ilibidi yatimizwe ili kumuunga mkono Uhuru, kwake siasa ni biashara, Kilicho muhimu katika uchaguzi huu ni suala la tabia, je William Ruto na mgombea mwenza wake Gachaguani ni watu wa aina gani? au Raila Odinga na Martha Karua?”

Uchaguzi mkuu wa Kenya unatajiwa kufanyika Agosti 9, 2022 ikiwa vinara wa uchaguzi huo ni William Ruto na Raila Odinga, ikiwa Mgombea aliyekonga nyoyo za watu katika kampeni ni Wajackoyah.

Majeruhi ajali ya King David wapewa rufaa
Mke wa Rais ahojiwa kwa Rushwa