Wananchi Kijiji cha Kilando kata ya Kilando Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, wamewasilisha kilio chao kwa Serikali juu ya bei kubwa ya Mafuta ya Petrol na Diesel na kuomba ifanyike tathmini ya kina ili kuwaokoa na adha hiyo.

Wananchi hao, wamewasilisha kilio chao kupitia kwa Waziri wa Nishati, January Makamba ambaye bado yupo kwenye ziara ya Kijiji kwa kijiji yenye lengo la kukagua, Kufatilia na kutatua kero za Wananchi kwenye sekta ya Nishati.

Mwananchi akiongea mbele ya Waziri wa Nishati, Ja

Akijibu hoja hiyo, Waziri Makamba amewasihi Wananchi hao kuendelea kuwa na imani na Serikali  kwakuwa bado wanaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha bei ya mafuta nchini inapungua.

Amesema, “Kuhusu suala la Mafuta ni lazima tujue sisi ni Wahanga wa bei ya Mafuta Duniani, endeleeni kuwa na imani na Serikali  kwakuwa bado inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha bei ya mafuta inapungua.”

Waziri Makamba ameongeza kuwa, pamoja na gharama za Mafuta Duniani kuwa juu, lakini bado Tanzania ndio nchi inayouza nishati hiyo kwa gharama ndogo zaidi ikilinganishwa na nchi zingine za Afrika. 

“Tumshukuru Rais Samia, bila ruzuku ya Bilioni 100 anayoitoa kila mwezi bei ya Mafuta ingekua imeongezeka shilingi 500 kwa kila lita ya Diesel na 200 kwa kila lita ya Petrol,” amefafanua Waziri Makamba.

Ziara ya siku 21 ya Waziri wa Nishati, January Makamba kupita Kijiji kwa Kijiji kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi juu ya changamoto za Nishati, inaendelea nchini na safari hii atakua Mkoani Mbeya.

Mwenyekiti Kamati ya Maadili amjibu Haji Manara
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 27, 2022