Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, John Heche amesema suala la Katiba mpya halikwepeki kwani litasaidia kuibadilisha nchi kiuchumi na kimaendeleo kwani katiba iliyopo inachangia ongezeko la umasikini.

Heche ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na Dar24 Media na kuongeza kuwa tatizo la nchi si watu au vitu, bali aina ya uongozi uliopo ambao hausaidii kusonga mbele na kwamba upo umuhimu wa kugatua madaraka.

Amesema, “suala la Rais kuwa na madaraka makubwa ya ugawaji wa mamlaka na amri ya kipi kifanyike na wapi, ni jambo ambalo linachangia kudidimizaji uchumi wa nchi na ndio maana sisi CHADEMA tunamini katika mgawanyo majimbo ambao utasaidia kufanikisha mambo mengi.”

Aidha, ameongeza kuwa, uwingi wa viongozi ambao hauna tija na ugawaji wa madaraka kwa watu wengi ambao hawana maono ya kitaifa unachangiwa na mfumo wa chama kilichopo madarakani unaoongozwa na watu wasio na uchungu na rasilimali za Taifa.

Serikali yaeleza sababu uchelewaji fidia kwa Wananchi
Utawala bora pekee hautoshi kuwahudumia wananchi - Othman