Dawa aina ya Remdesivir ambayo mara ya kwanza ilitengenezwa kutibu ugonjwa wa ebola, imetangazwa kuonesha matumaini ya kutibu ugnjwa wa covid 19.
Majaribio ya dawa hiyo yalisimamiwa na taasisi ya Marekani kuhusu uzio na magonjwa ya maambukizi NIAID.
Ni dawa ya kukabiliana na virusi na inafanya kazi kwa kushambulia enzymes ambazo virusi vinahitaji ili kuweza kuzaana ndani ya seli ya mwili wa mwanadamu.
Dkt. Anthony Fauci ambaye anaongoza Shirika la NIAID amesema “Data inaonyesha kwamba Remdesivir ina nguvu za wazi kwamba inaweza kupunguza dalili na kusaidia mtu kupona kwa haraka”.