Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo amefafanua kuwa serikali haijatoa ukomo wa wachezaji kutoka nje kushiriki michezo hapa nchini bali imeibua mjadala kwa wadau ili watoe maoni yao.

Singo ametoa ufafanuzi huo, kufuatia baadhi ya wadau wa soka nchini kuijadili kwa mtazamo tofauti kauli iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harriosn Mwakyembe kuhusu idadi ya wachezaji wakigeni wanaocheza kwenye klabu za ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Mwakyembe aliibua hoja hiyo kwa lengo la kutoa nafasi kwa wachezaji wazawa kucheza mara kwa mara kwenye klabu zao, tofaiti na sasa ambapo asilimia kubwa ya makocha wamekua wakiwatumia wachezaji wa kigeni kwenye vikosi vya kwanza, hususan klabu za Simba SC, Young Africans na Azam FC.

Singo amesema Waziri Mwakyembe hakushinikiza hoja hiyo ipitishwe ama kukubaliwa na mamlaka ya soka nchini TFF ambayo ilipitisha kanuni ya usajili wa wachezajui kumi wa kigeni, bali ameweka mjadala wazi ili kupata maoni tofautia mbayo yatajenga hoja hiyo na kuwa na mashiko.

Amesema suala la usajili wa wachezaji wakigeni limekua na mkadala wa muda wa mrefu, na halijaanza jana wala juzi, na alichokifanya Waziri Mwakyembe ni kutoa hoja ambayo anaamini kama itajadiliwa na kuonekana inafaa basi ifanyiwe marekebisho, na kama haitafaa basi kanuni ya usajili wa wachezaji wa kigeni itapaswa kuachwa kama ilivyo.

“Hili suala limekua na mjadala wa muda mrefu zaidi ya miaka mitatu /minne, ni mjadala mzito kwa sababu pande mbili zinazobishana unakuta zinatofautiana kidogo sana hasa linapokua suala la athari zake, kwa kuwa na wachezaji wa kigeni na kwa idadi gani,”

“Wapo wanaomuwekea maneno mdomoni Mh. Waziri, kwa sababu hakuongelea idadi, hakuelekeza ni idadi ya wachezaji wangapi wanahitaja, ila alilolifanya ni kufungua mjadala kwa kuilekeza Baraza La Michezo La Taifa (BMT), kufanya madajala wa wazi na kukusanya maoni, ili kuona ni jinsi gani wadau watachangia idadi ya wachezaji.” Alisema Singo

Singo amesema Tanzania haiwezi kuiga mfumo wa nchi fulani kuhusu kanuni ya usajili wa wachezaji wa kigeni, kutokana na kutambua kila nchi ina falsafa zake katika kanuni hiyo ya wachezaji wa kigeni, na zipo nchi zimegfanikiwa na nyingine kusindwa kufikia malengo.

“Kwa mfano nchi kama Uingereza falsafa yao ni kuhakikisha kwamba michezo inakua biashara, kwa hiyo walichokifanya ni kuhakikisha wachezji wote wazuri duniani wanakwenda kwenye nchi yao ili kuiwezesha ligi yao kuwa ligi bora. Kuvutia biashara, uwekezaji na mashabiki.”

“Pamoja na falsafa hiyo ya Uingereza, wamekua na athari kubwa ya kutokua na timu nzuri ya taifa kwa muda mrefu na ndio maana wameshindwa kutwaa mataji makubwa ya dunia.” Aliongeza Singo.

Mwisho Singo amesema Waziri Mwakyembe anataka kuona Baraza La Michezo La Taifa (BMT) linatoa fursa kwa wadau kutoa maoni yao kwenye mjadala wa wazi, ili kupata njia nzuri itakayowezesha hoja yake kuwa na mashiko.

Paris Saint-Germain yakabidhiwa ubingwa 2019/20
Tumaini laonekana dawa ya corona Marekani