Usiku wa Agosti 20 mwaka huu, iliweka historia nyingine kwenye utoaji wa Tuzo za Video za Muziki za MTV (MTV – VMAs) zilizofanyika New York nchini Marekani.
Wasanii wa kike walionekana kutawala tuzo hizo jana, wakizoa tuzo kubwa zaidi kama video bora ya mwaka na msanii bora wa mwaka (Camila), Video ya Wimbo bora wa Hip Hop (Nicki Minaj), Msanii Bora Mpya (Cardi B).
Katika tuzo hizo, Cardi B alikuwa anaongoza kwa kutajwa kwenye vipengele 10 akiwa nyuma ya Jay Z na Beyonce ambao walikuwa wametajwa kwenye vipengele 8 na Drake kwenye vipengele 7.
Tumekuandalia orodha ya washindi wa tuzo hizo kwenye vipengele muhimu.
Video ya Mwaka
Camila Cabello ft. Young Thug – “Havana” – Syco Music/Epic Records
Msanii Bora wa Mwaka
Camila Cabello
Wimbo Bora wa Mwaka
Post Malone ft. 21 Savage – “rockstar”
Msanii Bora Mpya
Cardi B
Ushirikiano Bora
Jennifer Lopez Feat. DJ Khaled na Cardi B – “Dinero”
Wimbo Bora wa Pop
Ariana Grande – “No Tears Left to Cry”
Wimbo Bora wa Asili ya Kilatini
J Balvin, Willy William — “Mi Gente”
Wimbo Bora wa Hip-Hop
Nicki Minaj – “Chun-Li”
Video Bora yenye Ujumbe
Childish Gambino – “This Is America”
Video yenye Uongozaji Bora
Childish Gambino – “This Is America”
Video yenye uchezaji bora (Choreography)
Childish Gambino – “This Is America”
Video Bora Kwa kuhaririwa (edited)
N.E.R.D & Rihanna – “Lemon”
Video Bora ya Msimu wa Kiangazi
Cardi B, Bad Bunny & J Balvin – “I Like It”