Baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya uchaguzi nchini Liberia, Rais George Weah na mpinzani wake Mkuu, Joseph Boakai wamevutana vikali kwa kura, huku Weah akipata kura 43.83%, Boakai, aliyekuwa makamu wa Rais, akijizolea kura asilimia 43.44.
Uchaguzi wa Oktoba 10, 2023 ulikuwa wa ushindani mkali zaidi wa urais nchini Liberia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe miongo miwili iliyopita ambapo Boakai mwenye umri wa miaka 78, akikaribia kura za Weah na hivyo kufanya duru ya pili ya uchaguzi kuwa ya kusisimua zaidi.
Hatua hiyo, inatokana na ukweli kwamba hakuna mgombeaji aliyepata zaidi ya 50% ya kura katika duru ya kwanza na Duru ya pili ya uchaguzi imepangwa kufanyika Novemba 14, 2023 kulingana na Kiongozi wa Tume ya uchaguzi, Davidetta Browne.
Boakai alimpita Weah katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa 2017, lakini alishindwa kwa kura nyingi katika kura ya mchujo.