Rais wa Malawi, Peter Mutharika anaongoza katika matokeo ya kura zilizohesabiwa hadi sasa na Tume ya Uchaguzi nchini humo ambapo tayari asilimia 75 ya kura zote zilizopigwa zimehesabiwa. Mutharika amepata asilimia 40.44 ya kura hizo zilizohesabiwa.
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Tume ya Uchaguzi, chama cha upinzani cha Malawi Congress Party chini ya mgombea wake Lazarus Chakwera ambacho awali kilikuwa kinaongoza kwa wingi wa kura, kwa sasa kimepata asilimia 35.34 huku makamu wa Rais Saulos Chilima akiwa na asilimia 18.35.
Alhamisi, Mei 23, kiongozi wa upinzani, Lazarus alikuwa anaongoza baada ya chama chake cha MCP kujipatia asilimia 37. 65 ya kura, huku akifuatiwa kwa karibu na Rais Mutharika aliyekuwa na asilimia 37.1.
Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi nchini humo imetoa wito kwa wananchi na wagombea kuwa watulivu ikisisitiza kuwa ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza matokeo rasmi.
Uchaguzi mkuu wa Malawi umekumbwa na ushindani mkali kati ya Rais Peter Mutharika, makamu wake Saulos Chilima na mgombea wa chama cha upinzani chenye nguvu Malawi cha Malawi Congress Party, Lazarus Chakwera.
-
Umoja wa Ulaya watoa tamko baada ya May kujiuzulu
-
RC atoa sababu ya kukusanya ATM kadi za watumishi
-
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 25, 2019