Vyama vya upinzani nchini Nigeria, vimejiondoa katika mchakato wa kuhesabu kura kutokana wasiwasi wa udanganyifu, huku mgombea wa chama tawala, Bola Tinubu akiongoza katika matokeo ya awali ya majimbo 15 kati ya 36.
Hesabu ya matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi – INEC, yalionesha Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC), alikuwa mbele kwa kura milioni 4.26, dhidi ya Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha People’s Democratic Party (PDP), chenye kura milioni 3.26.
Mgombea Peter Obi wa chama kidogo cha Labour, alikuwa katika nafasi ya tatu kwa kupata kura milioni 1.77 huku zoezi la kuhesabu kura likiingia katika siku yake ya pili hii leo Februari 28, 2023, kufuatia kumalizika kwa upigaji kura hapo jumamosi Februari 25, 2023.
Hata hivyo, haguzi huo umekumbwa na matatizo kadhaa ikiwemo ya vifaa na teknolojia hivyo kusababisha kukosekana kwa matokeo katika vituo vingi vya kupigia kura, na kupitia tovuti ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), imeahidi kufanyia kazi pungufu hilo ili kuhakikisha uwazi unakuwepo.