Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS) zinaonesha kuwa Uchumi wa Tanzania umekuwa kutoka asilimia 4.4 hadi asilimia 5.2, katika kipindi cha cha robo ya tatu ya mwaka 2021.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Takwimu za Uchumi Daniel Masolwa, wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma.

Masolwa, amefafanua kuwa Shughuli za Ujenzi, kilimo na uchimbaji wa madini ni kati ya sababu za ukuaji wa Uchumi wa asilimia 5.2.

Kwa mujibu wa Masolwa, nchi jirani za Afrika Mashariki zilizotoa ripoti zao ni Rwanda ambayo uchumi wake umekuwa kwa asilimia 10.1 na Uganda ambayo uchumi wake umekuwa kwa asilimia 3.8.

Dili la Chiko Ushindi lazimwa Young Africans
Jason Derulo awatembezea kichapo mashabiki