Kocha Mkuu wa klabu ya Young Africans Nasreddine Nabi amesitisha mpango wa usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo na klabu ya TP Mazembe Chico Ushindi.

Chico alitajwa kuwa kwenye mpango wa kusajiliwa kwa mkopo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la usajili ambacho kitafungwa rasmi Januari 15.

Kabla ya kuondoka nchini Kocha Nabi aliutaka Uongozi wa Young Africans kusitisha mpango wa kusajiliwa kwa mchezaji huyo, kufuatia gharama yake ya usajili wa mkopo kuwa kubwa, tofauti na ilivyotarajiwa.

Akizungumzia maamuzi hayo Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema: “Gharama yake kumchukua kwa mkopo wa mwaka mmoja unaweza ukawasajili mastaa wengi kama Mayele, sasa sijaona sababu ya kumsajili, pia naepusha migogoro ya wachezaji wengi kuanza kujiuliza mbona huyu ana gharama kubwa.”

Tayari Young Africans imeshafanya usajili wa wachezaji kadhaa katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, kwa lengo la kuongezea nguvu kwenye kikosi chao ili kutimiza lengo la kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Pablo: Tatizo la Penati Simba SC nitalimaliza
Uchumi wa Tanzania Umepanda