Tiketi ya timu ya taifa ya Ureno kuendelea kutetea ubingwa wa Fainali za Uefa Euro 2020, ipo mikononi mwa Ufaransa, ambao watakuna nao kesho Jumatano (Juni 23), kwenye uwanja wa Puskás, mjini Budapest nchini Hungary.
Ureno wanahitaji ushindi kwennye mchezo huo, ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo, na kuendelea kutetea taji lao, kinyuma na hapo watakua wamejiweka kwenye mazingira magumu.
Katika msimamo wa kundi F, Ureno ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 3, ikitanguliwa na Ujerumani yenye alama 3 na Ufaransa ipo kileleni mwa kundi hilo kwa kumiliki alama 4, huku Hungary ikiwa na alama moja bada ya kupata sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Mabingwa wa dunia (Ufaransa) mwishoni mwa juma lililopita.
Wakati Ureno ikitarajia kupambana dhidi ya Ufaransa, kikosi cha Ujerumani kutapapatuana dhidi ya Hungary ambao pia wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.
Timu zilizojihakikishia kucheza hatua ya 16 bora ya fainali za Uefa Euro 2020 hadi sasa ni Italia, Wales, Ubelgiji, Denmark, Uholanzi, Austria, Jamuhuri ya Czech, England, Sweden na Slovakia.