Klabu ya Manchester City imewasilisha ofa ya Kwanza ya dau la Pauni milioni 100 kwenda Klabu ya Tottenham ili kuapata saini ya Mshambuliaji Harry Kane.

Manchester City wanemesema wako tayari kutoa dau hilo na kutoa mchezaji mmoja kwenda Klabu ya Tottenham ili tu kupata saini ya nyota huyo raia wa England.

Klabu hiyo ipo tayari kumjumuisha Katika dili hilo mmoja wa wachezaji wake kati ya Raheem Sterling, Aymeric Laporte na Gabriel Jesus.

Lakini mpaka sasa Klabu ya Tottenham bado haijaamua kumuuza Harry Kane, kutokana na Daniel Levy kusema kuwa anataka kumbakisha straika huyo, na anaendelea kumshawishi.

Ikumbukwe Harry Kane anataka kucheza michuano ya UEFA Champions League kwa msimu Ujao, lakini kwa sasa yuko katika michuano ya EURO hivyo hakuna mazungumzo yoyote yanaendelea na Klabu yake katika kipindi hiki Cha Mashindano.

Manchester City imesema haitakata tamaa kusaka saini ya nyota huyo, kutokana na Pep Guadiola kusema kuwa anahitaji mbadala wa Sergio Aguero ambaye ameondoka.

source (Fabrizio Romano)

UEFA EURO 2020: Bingwa mtetezi mtegoni
Azam FC yajitoa mbio za ubingwa