Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) lipo kwenye mchakato wa uchunguzi wa vitendo vya kibaguzi vilivyotokea kwenye michezo miwili ya michuano ya Euro 2020.

UEFA imeanza kufanya uchunguzi huo baada ya kubaini kulikua na viashiria vya kibaguzi kwenye michezo hiyo iliyochezwa kwenye nchi ya Hungary mwishoni mwa juma lililopita.

Kwenye mchezo kati ya wenyeji Hungary dhidi ya Ufaransa uliopigwa Jumamosi (Juni 19), mashabiki wa timu mwenyeji waliingia na mabango kwenye dimba la Puskas Arena yakiwa na ujumbe wa kuwakataza wachezaji kupiga goti ili kupinga ubaguzi.

Pia Wachezaji wa Ufaransa Kylian Mbappe na Karim Benzema walifanyiwa vitendo vya kibaguzi.

Mashabiki wa Hungary wanapigiwa kelele za milio ya nyani pindi wachezaji hao walipogusa mpira.

Mkutano Baraza la Mawaziri EAC waanza, EACO sasa kurasimishwa
Mbeya City yaitangazia vita Simba