Kikosi cha Mbeya City Fc kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam, tayari kuwakabili Mabingwa wayeyezi wa Ligi Kuu Simba SC kesho Jumanne (June 22).

Mbeya City wanapambana kutokushuka daraja msimu huu, watautumia mchezo huo wa utakaochezwa kuanzia saa moja usiku, kama sehemu ya kuendelea kupambana kwenye vita ya kulikataa shimo la kushuka daraja.

Nyota 25, benchi la ufundi na watumishi wengine wa klabu waliwasili jijini Dar mapema Jumamosi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba SC.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa habari wa Mbeya City Shah Mjanja, wachezaji wote wa klabu hiyo ya jijini Mbeya wapo vizuri, isopokua Babilas Chitembe na Ally ‘Batezi’ Mtinge ambao kwa sababu tofauti tofauti hawawezi kushiriki.

“Wachezaji wote wapo salama, tunamshukuru mungu hali zao zinaridhisha kuelekea pambano letu la kesho dhidi ya Simba SC.” amesema Shah Mjanja.

Mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine, Simba SC iliitandika Mbeya City bao moja kwa sifuri, likifungwa na.mshambuliaji na nahodha wao John Bocco.

Mbise afunguka ya moyoni
Mbunge alia na Bureau De Change