Mbunge wa Jimbo la Gando Salimu Mussa Omar ameishauri serikali kupunguza mtaji wa kufungua  Bureau De Change ambapo ameiomba wizara ya fedha kuangalia tena swala hilo li kukuza uchumi wa nchi

Amesema hayo leo Juni 21, 2021 bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali

Amesema kuwa unapofunga moja kati ya viunganishi vya biashara unawaua kiuchumi wafanya biashara.

”Unapofunga moja kati ya Componet… za biashara unatuua kiuchumi unapoweka kizingiti katika biashara kama ya Bureau De Change unaua kabisa, hainiingii kichwani mwangu kuweka sh. milioni 300 mtaji wakufungua Bureau De Change…” amesema Mbunge Omary

Hata hivyo alipata taarifa kutoka kwa mbunge Jesca iliyosema kuwa ”Capital requiment ya kuanzisha Bureau De Change ni billioni 1 na sio millioni 300 na sio kama alivyosema hiyo ilikuwa ni ya awali”

Mbeya City: Tupo tayari kuivaa Simba SC
Waziri Ummy awataka Wakuu wa Mikoa kusimamia ukusanyaji mapato