Ikiwa ni miaka 23 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari, Ufaransa imeanzisha uchunguzi dhidi ya benki ya BNP Paribas kufuatia madai kuwa ilihusika na mauaji hayo nchini Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuawa.
Mashirika matatu ya umma yamepeleka kesi mahakamani dhidi ya benki hiyo yakiituhumu kwa kosa la kupitisha dola milioni 1.3 kwa muuza silaha.
Pesa hizo zilitumiwa kununua silaha jambo ambalo lilikiuka azimio la marufuku ya silaha la Umoja wa Mataifa wakati Kanali wa kabila la Hutu ambaye alipokea silaha hizo Theoneste Bagosora mpaka sasa bado anatumikia kifungo cha miaka 35 jela kwa uhalifu dhidi ya binadamu.
-
Sita washambuliwa kwa tindikali
-
Trump aongeza vikwazo Korea Kaskazini, Kim Jong-un ajibu
-
Auwawa akipambana na Polisi
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalizuka baada ya kushambuliwa kwa ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu tarehe 6 mwezi Aprili mwaka 1994.
Baada ya kuuawa kwa Rais Juvenal Habyarimana wanamgambo wa Hutu waliwaua watu wa Tutsi waliokuwa wachache katika kipindi cha siku 100.