Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wafugaji nchini kufuga kitaalam na kuacha ufugaji wa kuhamahama unaopunguza ubora wa bidhaa ya mfugo huku akisema Serikali itaendelea kufanya maboresho ya Sera ya Mifugo na Uvivu ili iweze kuleta tija kwa Taifa.

Majaliwa alisema hayo wakati alipotembelea maonesho ya wadau wa mifugo na uvuvi kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma na kuongeza kuwa, “tunajua tuna mafanikio na changamoto, lakini tunataka kuhakikisha Taifa hili linatumia bidhaa zitokanazo na mifugo na uvuvi, suala la masoko ya bidhaa zake ni pana.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema,”lengo la kufanya maboresho haya ni kuhakikisha sekta hiyo inaongeza mchango katika pato la Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja sekta ya mifugo na uvuvi ni muhimu sana, ni uchumi na mafanikio ya maisha ya kila siku ya anayejishughulisha na sekta hiyo.”

Awali, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega alimweleza Waziri Mkuu kuwa Kampuni ya ASAS inakusudia kujenga kiwanda cha kutengeneza maziwa ya unga, ambacho kitanunua maziwa yote na kuwaondolea wafugaji hasara hasa kipindi cha mvua ambapo uzalishaji wa maziwa unaongezeka.

Mshambuliaji KMKM azitaja Simba, Young Africans
Azam FC kumng'oa Peter Banda Simba SC