Serikali nchini Uganda, inapanga kutangaza awamu ya tatu ya utoaji leseni ya mafuta mwezi Mei, 2023 ikiwa ni juhudi za kuendeleza zaidi sekta ya uzalishaji wa mafuta yake ya kwanza mwaka 2025.
Waziri wa Nishati, Ruth Nankabirwa Ssentamu amesema awamu hiyo ijayo ya utoaji leseni itatangazwa katika mkutano wa kikanda wa mafuta ya petroli, unaotarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala mwezi Mei 2023.
Uganda, iligundua akiba ya hidrokabon za kibiashara karibu na mpaka wake wa magharibi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2006 huku uzalishaji hu ukitarajiwa kuanza mwaka 2025.
Aidha, nchi hiyo pia inajenga bomba la kusafirisha mafuta ghafi na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi cha ndani, ambacho kitasaidia kukuza rasilimali za mafuta na kujiinua kiuchumi kupitia biashara.