Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani ameagiza ya kuongezwa kwa uwajibikaji katika usimamizi na utekelezaji wa mipango mikakati itakayoandaliwa, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga, kudhibiti mimba na ndoa za utotoni.

Batilda ameyasema hayo katika ufunguzi wa kikao cha watalaam wa Afya Kanda ya Magharibi, inayounda mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga katika kanda hiyo.

Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Lebba akizungumza na wataalam wa Afya kanda ya Magharibi katika ufunguzi wa kikao hicho cha 
kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma.

Amesema, Kiwango cha mimba za utotoni kwa kanda ya Magharibi ni asilimia 25.2 kwa Mkoa wa Katavi, Tabora asilimia 17 na Kigoma asilimia 11.9 huku hudhurio la kwanza la wajawazito chini ya wiki kumi na mbili kwa mkoa wa Tabora likiwa ni asilimia 34.4, Katavi asilimia 41 na Kigoma asilimia 54.9.

Mkuu huyo wa Mkoa, amefafanua kwamba kiwango cha utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango kwa mkoa wa Katavi ni asilimia 41, Kigoma asilimia 46.4 na Tabora asilimia 60.1 hivyo kutaka elimu ya Afya itolewe kwenye jamii.

Mkunga Mbobezi toka Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga ,Wizara ya Afya, Aziza Machenje akichangia mada namna ya kufanya mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi na Watoto wachanga.

Aidha ameongeza kuwa, elimu hiyo itolewe kupitia njia mbalimbali za mikusanyiko ya watu, mashuleni, makanisani na misikitini, vyombo vya habari na kwamba wale wote wanaowapa mimba watoto wa shule sheria ichukue mkondo wake, ili kudhibiti vitendo hivyo.

Uganda kutangaza awamu mpya utoaji leseni za uzalishaji wa mafuta
Waziri wa zamani wa Nishati jela miaka 20 kwa ufisadi