Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema mtu anayedhibiti mbegu anaweza kukutawala na hata kukugeuza mtumwa kwakuwa ni rahisi kwake na ndiyo maana Serikali imeanzisha mamlaka ya afya ya mimea kisheria.

Bashe, ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Dar24 Media ofisini kwake jijini Dodoma, wakati akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua udhibiti wa mbegu toka nje ambao umekuwa unalalamikiwa na Wakulima kuwa hauna tija katika mazao.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Amesema, “anaye control mbegu ndiye anayekutawala na anayedhibiti mbegu pia anaweza hata akadhibiti chakula chako, hata mtu anayedhibiti mbolea naye anaweza kukutawala kwa sababu anao uwezo wa kufanya hivyo huo ndiyo ukweli.”

Aidha, Bashe amesema kutokana na hali hiyo, Serikali imeamua kuweka fedha ya kutosha kwenye utafiti na kuweka miundombinu ya kuzalisha mbegu kwenye mashamba 17 na kwamba malengo ya Serikali katika mwaka ujao wa fedha ni kujenga hekta 10,000.

Aina tofauti ya mbegu.

Hata hivyo, Waziri Bashe amesema si kweli kwamba Tanzania haina mbegu kwani watafiti wamefanya kazi kubwa kwa zaidi ya miaka 15 – 20 kutengeneza mbegu za msingi na ndiyo maana Serikali imeamua kuwekeza maeneo hayo.

Aidha amesema licha ya ukubwa wa nchi ya Tanzania, bado Serikali haitaruhusu sekta ya Kilimo kuchafuliwa na pia haitawezekana kujifungia ndani.

Mapambano vifo vya uzazi, watoto wachanga si ya Wizara pekee: Dkt. Batilda
Mashabiki, Wanachama Simba SC waombwa kubadilika