Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu, wamawataka baadhi ya Mashabiki na Wanachama kukubali wa klabu hiyo kubadilika na kwenda sambamba na mfumo wa Soka unavyotaka.

Mangungu ametoa rai hiyo, alipozungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Januari 20), wakati akizindua kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo, uliopangwa kufanyika Januari 29 jijini humo.

Kiongozi huyo amesema baadhi ya Mashabiki na Wanachama wamekua na fikra za kizamani na wakati mwingine humpigia simu binafsi wakimtaka kufanya maamuzi, ama kufikisha ujumbe kwa wahusika ndani ya Klabu hiyo, kitu ambacho kinapingana na mfumo wa soka la kisasa.

Mangungu ametolea mfano wa baadhi ya matukio aliyokutana nayo, akigusia mchezo wa juzi Jumatano (Januari 19), dhidi ya Mbeya City ambao ulimalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa 3-2.

“Mechi ya juzi na Mbeya City, Chama katoka na Bocco katoka lakini mtu anakupgia simu anakwambia ‘Mwambie huyo kocha kwanini Chama katoka’ baada ya goli la 2 la Mbeya City ananipigia simu ananiambia ‘Mwambie Aish Manula aache uzembe.

“Nikishuka jukwaani kwenda kwenye benchi uwanjani kwanza mimi nitafungiwa lakini klabu italipa faini mil 3 kwa mimi kufika uwanjani na mil 5 kama ningeenda vyumba vya kubadilishia nguo.”

“Sasa hivi mfumo umebadilika tusikariri yale mambo ya mwenyekiti kuingia uwanjani kuhamasisha wachezaji hayo mambo hayapo timu inaenda kwenye professionalism.” amesema Mangungu

Mangungu anatetea nafasi yake klabuni hapo sambamba Moses Stewart Kaluwa, baada ya Kamati ya Uchaguzi kuwapitisha wawili hao kuwania nafasi ya Mwenyekiti upande wa Wanachama.

Anayedhibiti mbegu anaweza kukutawala: Bashe
Fiston Meyele amkosha Kennedy Musonda