Mshambuliaji mpya wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Kennedy Musonda, amekiri kukoshwa na uwezo wa Mshambuliaji mwenzake Fiston Kalala Mayele.

Musonda alitambulishwa rasmi kwa Mashabiki na Wanachama wa Young Africans mwishoni mwa juma lililopita, baada ya kukamilisha taratibu za usajili wake klabuni hapo akitokea Power Dynamos ya nchini kwao Zambia.

Mshambuliaji huyo amesema baada ya kufanya mzoezi na kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu FC sambamba na Mayele, amejiridhisha Mshambuliaji huyo kutoka DR Congo ana uwezo mkubwa ambao utaendelea kuisaidia Young Africans.

“Tumepata nafasi ya kucheza kwa pamoja kwenye mchezo dhidi ya Ihefu FC na tulifanya mazoezi pamoja kabla ya mchezo huo, kwa maoni yangu naweza kusema hakuna namna ya kumuelezea zaidi ya kusema ni miongoni mwa washambuliaji hatari zaidi ambao nimewahi kucheza nao.”

“Naamini kadiri muda unavyozidi kusogea tutakuwa na muunganiko mzuri zaidi na nadhani tutafanya mambo makubwa pamoja.” amesema Musonda.

Musonda mwenye umri wa miaka 29, amejiunga na Young Africans, akiacha kumbukumbu nzuri katika Ligi Kuu ya Zambia, akifunga mabao 11 msimu huu 2022/23.

Mashabiki, Wanachama Simba SC waombwa kubadilika
Clatous Chama awakana mashabiki Simba SC