Nchini Uganda wagonjwa wapya 13 wa virusi vya corona wameongezeka na kufanya visa nchini humo kufikia 139, wakiwemo madereva wa malori waliothibitika baada ya sampuli 1,741 za Covid 19 kupimwa jana Mei 13, 2020.

Wizara ya Afya imeeleza kuwa jumla ya sampuli zilizopimwa jana ni 2,104 ambapo sampuli 363 zilikuwa za Wananchi katika jamii
mbalimbali nchini humo na zote zilikutwa hazina maambukizi.

Hata hivyo kati ya Wagonjwa hao wapya, Waganda ni 7, Wakenya ni 5 na mmoja ni raia wa Eritrea ambao wanaelezwa kuingia Uganda wakitokea Tanzania, Sudan Kusini na Kenya kupitia mipaka ya Mutukula, Elegu na Malaba.

Hivi karibuni Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki waliokutana walikubaliana kuwa madereva wa malori watakuwa wakipimwa mara mbili, watapimwa nchi watokako na wataondoka ikiwa wako salama na pia watapimwa nchi wanakoenda.

Hija Ugando: Nilishindwa kucheza Tunisia, Italia
WHO: virusi vya corona vinaweza visiishe kama ilivyo UKIMWI