Serikali ya Uganda imekashifu uamuzi wa Marekani kuongeza vikwazo vya viza dhidi ya maafisa wake, ikiishutumu Washington kwa kushinikiza ajenda ya ushoga barani Afrika.
Waziri wa mambo ya nje wa Uganda, Okello Oryeme, amesema kitendo cha Marekani ni wazi kinaashiria kushinikiza ajenda ya ushoga kwa mataifa ya Afrika, akihoji kwanini hatua kama hizi hazichukuliwi kwa mataifa mengine ya mashariki ya kati yenye sheria kama yao.
Vikwazo hivi vipya vilivyotangazwa vinalenga maafisa wasiojulikana ambao Marekani inawaona wanawajibika kudhoofisha demokrasia na kukandamiza makundi yaliyotengwa nchini Uganda, ikiwa ni pamoja na jumuiya ya LGBTQ.
Mradi USAID kuwanufaisha Vijana Moro
Uganda ilipitisha moja ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya mashoga mwezi Mei, ambayo inatoa hukumu ya kifo kwa watakaobainika kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, Sheria hii imeibua wimbi la unyanyasaji dhidi ya ushoga.
Vikwazo vya Marekani, vinaenda sambamba na vile vya Benki ya dunia ambayo ilitangaza kusitisha misaada yake kwa nchi hiyo.