Katika kisa cha kutatanisha huko Kisii Nchini Kenya, familia moja (majina yanahifadhiwa), imejikuta ikiwa haina makazi baada ya nyumba yao kuharibiwa katika mzozo kati ya Mke mdogo na Mkubwa walioolewa na Mwanamume mmoja.
Katika kisa hicho, inadaiwa kuwa, watoto kutoka kwa ndoa ya kwanza ya Mwanamume (Nyumba kubwa), walikula njama na kwenda kufanya uharibifu huo, huku ikidaiwa kuwa sababu kuu ya mzozo huo ni upendeleo wa huduma.
Inaarifiwa kuwa Baba wa familia hizo amekuwa akiipendele nyumba ndogo, huku familia ya kwanza ikidai kuwa pia hutumia muda mwingi katika nyumba hiyo iliyoharibiwa na wao kupuuzwa.
“Wanamtuhumu Baba yao kwa upendeleo, wakitoa mfano ambapo anadaiwa kununua nyama ya mke wa pili pekee huku mama yao mzazi akiachwa na mlo wa kila siku wa sukuma wiki bila mafuta ya kula,” alisimulia shuhuda mmoja.