Ugonjwa ulioikumba Timu ya Taifa ya Ufaransa mwanzoni mwa juma hili unaendelea kusambaa kwenye kambi ya timu hiyo huko nchini Qatar.

Awali Wachezaji Adrien Rabiot na Dayot Upamecano waliripotiwa kukabiliwa na ugonjwa huo wa ajabu, lakini taarifa mpya zinaeleza kuwa Kingsley Coman amepatwa homa na alikosa mazoezi ya jana Alhamis (Desemba 15).

Taarifa hizo zimeeleza kuwa, Coman alianza kujihisi vibaya kabla ya mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Morocco uliopigwa juzi Jumatano (Desemba 14).

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Kikosi cha Ufaransa Didier Deschamp, amesema dalili za ugonjwa huo huanza kwa mtu kujihisi vibaya na baadae kupata mafua yanayoambatana na homa pamoja na kuumwa koo.

“Joto limepungua kidogo Doha, na bado tuna viyoyozi wakati wote, nafikiri hii ndio inaleta hali ya mafua”. amesema Deschamp

Hata hivyo Wachezaji Rabiot na Upamecano wanaendelea vizuri na wana nafasi kubwa ya kuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kitakachoikabili Argentina keshokutwa Jumapili (Desemba 18) katika mchezo wa Fainali.

FPF, Santos wavunja mkataba rasmi
PICHA: Simba SC yawasili salama Mwanza