Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaonya viongozi wa vyama vya siasa nchini wanaoingiza  vijana kwenye mambo ya uhalifu kuendelea kupambana na siasa na si uhalifu.

Akizungumza leo Oktoba 9,2020 jijini Dar es salaam, IGP Sirro, amesema kuwa uhalifu hauwezi kuwafanya wao kuwa viongozi huku akidai kuwa uwepo wa baadhi ya wananchi wachache walioandaliwa kufanya vurugu.

“Niwaombe sana wanasiasa pambaneni na mambo ya siasa msijaribu kuingiza vijana kwenye mambo ya uhalifu, uhalifu hauwezi kukufanya ukawa kiongozi sanasana mnawaharibia vijana maisha yao, maarifa yao, mwisho wa siku wanapata adhabu wanafungwa wanaacha familia zao” amesema IGP Sirro.

“ Niwaombe sana pambaneni na siasa muweze kuwa viongozi lakini msitiumie vijana kuwaingiza kwenye uhalifu wakipata shida na familia zao wakati nyinyi mnaenjoy maisha na familia zenu” amesema IGP Sirro.

Hata hivyo IGP Sirro amewataka vijana kutokukubali kutumika vibaya na viongozi wa siasa badala yake wawaache wafanye uhalifu wenyewe ili wapambane na sheria zilizopo.

Vitambulisho vya wajasiriamali kutumika kukata bima afya
Bweni la shule ya sekondari lateketea kwa moto