Wazazi na walezi Kijiji Cha Homari, Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, wametakiwa kuwa waangalizi wa karibu kwa watoto wao kuanzia wakiwa nyumbani ili kuzuia kujiingiza kwenye makundi mabaya na hatimae kupelekea kuwa wahalifu ama kuvunja sheria.

Hayo yamesemwa na Askari Kata ya Masakta Wilayani humo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Christina Mlomi wakati akizungumza na wazazi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho.

Amesema, “mtoto wako usimuache ajiamulie, mpangie ratiba na usione anarudi usiku halafu ukanyamaza, unapaswa kuchukua hatua kwani kwa kukaa kimya kunampelekea kujiunga na makundi mabaya.”

Aidha, Christina ameongeza kuwa watoto na vijana wengi huanza vitendo vya kihalifu wakiwa nyumbani hivyo alitoa wito kwa wazazi kuchukua hatua mapema ikiwa ni pamoja na kuwaadhibu pindi wanapobaini uwepo wa viashiria hivyo.

Hata hivyo, Elimu dhidi ya ukatili na masuala ya usalama inaendelea kutolewa kwa jamii katika maeneo yote mkoani humo, ili kuongeza uelewa wa dhana ya Polisi Jamii na miradi yake.

Mlipuko wa Bomu la kutegwa wauwa sita Sokoni
Trump ni tishio kwa Demokrasia - Biden