Rais wa Marekani, Joe Biden, amezidisha mashambulizi yake dhidi ya rais wa zamani na mgombea anaeongoza katika chama cha Republikan, Donald Trump akidai kuwa ni kitishio kwa desturi na taasisi za kidemokrasia za nchi.

Katika hotuba yake aliyoitoa jimbo la magharibi la Arizona, Rais Biden amemshutumu Trump kwa kuwa na dhana za hatari kwa kuona kuwa anayo nguvu isiyosimamiwa na yupo juu ya sheria na madai yake kuwa katiba inampa haki ya kufanya chochote anachotaka kama rais.

Aidha, Rais Biden amesema hajawahi kusikia rais akiwa anasema hivyo isipokuwa Mwaka 2019 ambapo Trump alisema kwamba ana haki hiyo chini ya ibara ya pili ya katiba ambayo inazungumzia madaraka ya rais.

Mapema mwezi Machi 2023, Trump aliwaeleza wafuasi wake kwamba yeye chaguo sahihi na ni haki yao kuwa kiongozi wao na wote ambao wamekuwa wakifanyiwa mabaya yeye ndiye mtetezi wao.

Uhalifu: Wazazi, Walezi wapewa mbinu kuwalinda Watoto
Nendeni mkasikilize kero za Wananchi - Dkt. Biteko