Idara ya Uhamiaji imetangaza rasmi uzinduzi wa huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni (Online Passport Application Form), huduma hiyo kuanza rasmi siku ya Jumatatu ya tarehe 7 Agosti, 2017.
Na inapenda kuwatangazia Umma kuwa huduma hiyo itapatikana kupitia tovuti yao ya https://www.immigration.go.tz/ppt_application/.
Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo, imeawaomba waombaji wote wa pasipoti kujaza fomu hizo mtandaoni kisha kuzichapisha na kuziwakilisha katika ofisi za uhamiaji.
Hata hivyo, matumizi ya huduma hii yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo.
-
Kinana ampa tano Museven, asema hakuna Rais duniani kama yeye
-
JPM awataka wapinzani mkoani Tanga kutojisifia
Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma waombaji wameshauriwa kutembelea anuani ya Idara ambayo ni info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao.