Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema kuwa hakuna Rais duniani kote ambaye awewahi kuja Tanzania mara nyingi na mkoa wa Tanga kama Rais Museveni.

Ameyasema hayo mapema hii leo katika sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta katika eneo la Chongoleani Tanga ambapo amesema kuwa Rais Museveni ni ndugu yetu na si rafiki wa Tanzania

“Hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanzania mara nyingi kama Museveni, hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanga mara nyingi kama Museveni, alikuwa akitusihi sana kujenga reli hapa Tanga  ila leo naona anafuraha kwamba reli haikuwezekana lakini bomba la mafuta limeonekana, lakini nampongeza sana Rais Dkt. Magufuli kwa sera zao nzuri na vyama vyao kuwezesha bomba la mafuta,”amesema Kinana

Aidha, Kinana amesema kuwa amemsikia Rais huyo wa Uganda akisema kuwa Tanzania na Rwanda ni nchi ndugu na si marafiki, lakini yeye amsema kuwa naona Rais Magufuli na Museveni wote wana sera moja ya  siasa ni uchumi na uchumi ni siasa.

Hata hivyo, kwa upande wake Rais Museven amesema kuwa Watanzania si rafiki zake bali ni ndugu zake hivyo wakimkubalia atafurahi sana hata wasipomkubali yeye atabaki kuwa ni ndugu.

Mkuu wa Wilaya awasweka ndani wajumbe wa bodi ya Mkula
Ndoa ya Irene Uwoya nayo mbioni kusambaratika