Mgombea Urais wa Chama cha UDA, William Rutto amemkashifu Rais Uhuru Kenyatta kwa kuasi wandani wake wa zamani katika ngome yake ya Mlima Kenya na kuwakumbatia wale aliodai kuwa maadui wake wa kisiasa waliompinga na kumthalilisha huko nyuma.
Ruto ameyasema hayo wakati akinadi sera zake kwa mara ya mwisho katika eneo hilo, wakati wananchi wakijiandaa na Uchaguzi mkuu Agost 8, 2022.
Amesema, kutokana na uasi huo ana imani thabiti kuwa atajizolea kura nyingi katika eneo hilo na kupunguza umaarufu wa Odinga Mlimani.
”siku hizi Uhuru hajui hata nani amempigia kura nani hakumpigia kura, fikiria sasa hivi Uhuru anafikiri sisi ndiyo maadu zake eti Raila ndiyo rafiki wa Uhuru si hii ni maajabu…!ni maajabu au si maajabu jamani”. amesema Ruto
Eneo la Mlima Kenya lina zaidi ya wapiga kura milioni nne, huku Naibu Rais William Ruto akipuuzia mbali juhudi za kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga kupenya mlima Kenya.
Aidha Ruto amewaahidi wakazi wa Kaunti ya Nyeri kuwa ataleta mabadiliko katika sekta ya kilimo ambayo ndiyo kitega uchumi ambacho kinachotegemewa na wakazi wengi.